MYTH
Ikiwa umeshapata matibabu ya FGS, unakuwa umelindwa maisha yako yote.
FACT
Kuambukizwa tena ni hali ya kawaida na matibabu ya awali haimaanishi kwamba mtu hawezi kuambukizwa tena. Unapaswa kutafuta matibabu kila wakati unapokuwa umetumia maji kutoka chanzo cha maji kilichoambukizwa. Hata hivyo, hatari ya kupata ugonjwa mkali inakuwa imepunguzwa na inaweza hata kubadilishwa matibabu yanapokuwa yametumiwa mara kwa mara tangu utotoni.