Dawa za kupunguza makali ya VVU ni hatari kwa afya yako.
FACT
Dawa za kupunguza makali ya VVU huimarisha afya yako na kulinda mfumo wako wa kingamwili. Bila dawa hizo utaugua. Iwapo madhara ya dawa yanakufanya uugue, mweleze mhudumu wako wa afya. Anaweza kukusaidia kutafuta suluhu.