MYTH
Mtoto hahitaji kupimwa VVU, ilimradi tu mama yake anatumia dawa za kupunguza makali ya VVU wakati wa ujauzito.
FACT
Watoto wote waliozaliwa kwa mama aliye na VVU wanapaswa kupimwa VVU. Wanatakiwa kupimwa wanapozaliwa au ndani ya siku mbili baada ya kuzaliwa, kisha wakiwa na umri wa wiki 4 hadi 6. Iwapo mtoto ananyonyeshwa, anapaswa kupimwa tena akiwa na umri wa miezi 9 na miezi 18 au miezi mitatu baada ya kuacha kumnyonyesha, lolote litakalotangulia.