MYTH
Tohara ya Hiari ya Kimatibabu kwa Mwanaume (VMMC) huondoa sehemu kubwa ya uume wako.
FACT
Tohara ya Hiari ya Kimatibabu kwa Mwanaume huondoa "safu ya juu" ya ngozi kutoka kwenye uume wako, inayoitwa govi. Haitabadilisha ukubwa wa uume wako au kile kinachoweza kufanywa na uume wako. Huondoa tu njia kuu ambayo VVU huingia mwilini mwako.