Boost

Matatizo ya afya ya akili yanaweza tu kupimwa na mtaalamu wa afya aliyepata mafunzo. Atahitaji kuelewa hali inayokukumba, kwa hivyo anaweza kukuuliza: a)Jinsi unavyohisi? b)Hisia hizo zinakuathiri vipi? Zinabadilisha mwenendo wako na shughuli unazofanya? c) Umekuwa na hisia hizo kwa muda gani?

Kulingana na maelezo utakayompatia, atakupa viwango tofauti vya utunzaji na usaidizi. Ni sawa kuelezea wasiwasi wowote ulionao kuhusu mtaalamu huyo. Anapaswa kujibu maswali yoyote uliyonayo. Watu tofauti huenda wakawa na mitazamo tofauti kuhusu kupimwa. Kwa mfano, Kwa baadhi ya watu, kupimwa afya ya akili kunaweza kuwa jambo zuri. Wanaweza kuhisi kuwa wamepata njia ya kuzungumza na kujifunza kuhusu matatizo ambayo wamekumbana nayo kwa muda fulani. Watu wengine wanaweza kuhisi kuwa kupimwa ni jambo rahisi na haliwezi kutoa majibu ya matatizo yanayowakumba. Wanaweza kuhofia watu watahisi hali hiyo imesababisha wawe jinsi walivyo. Ni sawa kuwa na mtazamo tofauti kuhusu kupimwa. Vipimo vinapaswa kukusaidia upate usaidizi sahihi na si kujaribu au kukuchukulia ulivyo kutokana na tatizo hili.


 

Kama yalivyo matatizo mengine ya kiafya, ugonjwa wa akili unaweza kusababisha unyanyapaa. Kumbuka kuwa unyanyapaa hutokana na kutokuwa na taarifa sahihi na kutoelewa. Mambo ambayo unasikia kuhusu ugonjwa wa akili mara nyingi si kweli na yanaweza kusababisha changamoto za maisha kwa watu wanaokumbwa na ugonjwa wa akili.

Katika suala la afya ya akili kuna unyanyapaa mwingi kuhusu tatizo hilo, unyanyapaa huo husababishwa na hali kwamba ugonjwa wa afya ya akili haulingani na matatizo mengine, ugonjwa huu hauna dalili zozote za kimwili, ikimaanisha kuwa haujulikani kirahisi. Hali kwamba matatizo ya afya ya akili si rahisi kubainika huwafanya watu waamini visivyo kuwa:

a) si ya kawaida b) si halisi au ni rahisi kupona c) hayana madhara makubwa kuliko magonjwa ya kimwili.

Ili kutatua matatizo ya unyanyapaa dhidi ya ugonjwa wa akili, kunapaswa kuwa na elimu bora zaidi kuhusu ustawi wa akili pamoja na huduma bora za afya kwa wale walio na ugonjwa huo.
 

Matatizo ya afya ya akili ni ya kawaida sana. Kulingana na takwimu, katika kila mwaka, mtu mzima mmoja kati ya wanne anakumbwa na matatizo ya afya akili. Yanaweza kuwa na madhara makubwa katika maisha ya watu, kama ambavyo magonjwa ya kimwili yanavyoweza kuathiri watu. Hata hivyo, kwa kupata utunzaji sahihi, watu wengi wanapona au kujifunza kuishi nayo na kuyadhibiti katika njia inayowafaa.


 

Inaweza kuwa vigumu kuona mtu unayemjali akiwa na changamoto ya kiafya na unaweza kukosa cha kufanya ili kumsaidia, lakini fahamu kuwa kwa kufanya vitu vidogo, kumpa msaada anapohitaji na kumsikiliza - kunaweza kumsaidia kwa kiasi kikubwa. Afya duni ya akili huathiri watu katika njia mbalimbali na watu tofauti wanaweza kuhisi wamethaminiwa kwa kuwapa aina tofauti za usaidizi. Mara nyingi kufahamu kuwa una mtu wa kuzungumza naye kunaweza kuwa jambo la muhimu. Inaweza kuwa vigumu kwa mtu anayetatizika na ugonjwa huo kuanzisha mazungumzo, kwa hivyo wasiliana naye na umuulize kuhusu hali yake. Mfahamishe kuwa upo tayari iwapo atahitaji kuzungumza lakini usimlazimishe iwapo hayupo tayari. Tambua kwamba anachokueleza kinaweza kuwa mambo ambayo asingependa kumweleza mtu mwigine yeyote.

Epuka kukisia hali aliyo nayo na usizungumze mambo ambayo yataonyesha kuwa unafikiri kutatua tatizo hilo ni rahisi. Kutiwa moyo kufanya kila jambo lionekane kawaida kunaweza kufanya watu wahisi wanakosea jinsi wanavyofanya. Ni muhimu kutambua kuwa matatizo ya afya ya akili ni halisi na kuwa kuishi nayo inaweza kuwa vigumu. Sikiliza jinsi wanavyohisi bila kuwachukulia vibaya.

Kila wakati unaweza kumuuliza jinsi ambavyo anaweza kuhitaji usaidizi. Watu tofauti wanaweza kuhitaji usaidizi tofauti. Baadhi ya watu wanaweza kuhitaji kuzungumza, wengine wanaweza kuhitaji usaidizi wa vitendo kwa mfano utunzaji wa watoto au miadi ya kiafya. Kwa ujumla, kutulia na kujaribu kufanya mambo yaonekane kawaida kunaweza kusaidia. Kuweza kuzungumza kuhusu mambo mengine tofauti na afya ya akili kunaweza kuwa muhimu. Kumbuka kuwa huwezi kufanya kila kitu. Kumsaidia mtu mwingine inaweza kuwa vigumu. Jitunze na upate mapumziko ukihitaji. Iwapo hutaweza kushughulikia mwenyewe unayopitia, angalia jinsi ya kupata usaidizi katika hali inayowafaa.