Je, watu walio na VVU wapo katika hatari zaidi ya kupata COVID-19?
Ushahidi wa sasa unaonyesha kwamba VVU si sababu kuu ya kufanya COVID-19 iathiri zaidi kuliko matatizo mengine ya kiafya, kama vile shinikizo la damu, ugonjwa wa moyo, ugonjwa wa mapafu, saratani, kisukari au kuwa na umri mkubwa zaidi. Hata hivyo watu walio na VVU ambao mfumo wao wa kingamwili umeathiriwa wanaweza kuwa katika hatari kubwa zaidi na wanapaswa kufuata hatua za ziada ili kuzuia kuambukizwa. Hii ni pamoja na watu wenye:
kiwango kidogo cha CD4(<CD4 200 /seli),
kiwango kikubwa cha virusi kwenye damu maambukizi ya hivi majuzi ya magonjwa nyemelezi. Njia bora zaidi ya kuimarika kiafya ni kupata matibabu ya kupunguza makalai ya VVU.
Watu walio na VVU wanawezaje kujizuia wasipate COVID-19?
Watu walio na VVVU wanapaswa kufuata ushauri wa jumla wa kuzuia COVID-19. Hii inajumuisha kukaa umbali wa mita 1 kutoka walipo wengine, kunawa mikono yako mara kwa mara, kuvaa barakoa na kufuata kanuni au ushauri wowote unaotolewa mahali ulipo. Iwapo una VVU, unaweza kuchukua hatua za ziada kulinda afya yako kwa sasa: 1. 1. Weka akiba ya dawa za kupunguza makali ya VVU. Unapaswa kuwa na dawa za kutosha nyumbani za kutumia kwa angalau siku 30 (ikiwezekana kwa miezi mitatu).
2. Hakikisha umepata chanjo hivi majuzi.
3. Pata ushauri kutoka kituo cha afya na wanarika kupitia simu au ujumbe.
4. Weka mikakati, ikiwa utaumwa au ukihitaji kusalia nyumbani, ikijumuisha jinsi utakavyopata chakula na dawa au wasiliana na kituo cha afya.
5.Imarisha afya kwa kula mlo kamili na kufanya mazoezi.
6. Zingatia afya yako ya akili. Wasiliana na marafiki na familia kupitia simu na upate usaidizi wa ziada ukihitaji.
Je, COVID-19 inaweza kuambukizwa kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto?
COVID-19 inaweza kuambukizwa kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto kwenye uterasi, lakini ni nadra sana. Wanawake wajawazito wanapaswa kuendelea kufuata ushauri wa kuzuia na kupata utunzaji wa kiafya mara tu wanapohisi wana dalili za COVID-19. Manufaa ya kunyonyesha huzidi hatari zozote za kumwambukiza mtoto COVID-19 . Kina mama walio na COVID-19 wanashauriwa kuendelea kunyonyesha mradi tu wanahisi wanaweza kufanya hivyo. Iwapo una COVID-19, unaweza kupunguza hatari ya kumwambukiza mtoto wako kwa:
1. kuvaa barakoa
2. kunawa mikono yako kabla na baada ya kumlisha mtoto
3. kutumia tishu ili kuziba mdomo wako ukihitaji kukohoa au kupiga chafya (tupa tishu mara tu baada ya kuitumia na unawe mikono yako).
Je, ninapaswa kuvaa barakoa katika maeneo ya umma?
Shirika la Afya Ulimwenguni linapendekeza kuwa watu wavae barakoa wanapotangamana na watu ambao si wanafamilia:
ukiwa ndani ambapo kuna mfumo duni wa hewa ukiwa ndani ambapo kuna mfumo wa hewa lakini huwezi kukaa umbali wa mita 1 kutoka walipo watu wengine. Ukiwa nje ambapo huwezi kukaa umbali wa mita
1. kutoka walipo watu wengine. Ikitegemea mahali ulipo ulimwenguni kunaweza kuwa na kanuni zingine zinazohitaji uvae barakoa katika hali fulani. Hakikisha unafahamu mapendekezo yanayotumika mahali unapoishi ili uyafuate. Sababu kuu ya kuvaa barakoa ni kuzuia kuambukiza wengine COVID-19. Watu wanaweza kuambukiza COVID-19 hata wakiwa hawana dalili zozote. Kuvaa barakoa pamoja na kukaa kwa umbali inapowezekana, kutasaidia kuzuia COVID-19 isisambae. Hata hivyo ikiwa una dalili za COVID-19 unapaswa kusalia nyumbani na ujitenge - kuvaa barakoa haitoshi.
Je, ni aina zipi za kufunika uso ambazo zinafaa zaidi kuzuia usambaaji wa COVID-19?
Kuna aina mbili kuu za barakoa: barakoa za vitambaa (ambazo unaweza kutengeneza mwenyewe) na barakoa za kimatibabu (ambazo ni chache na zinatakiwa kuhifadhiwa ili zitumiwe na wahudumu wa afya). Aina ya barakoa inayokufaa itategemea wewe ni nani na aina ya hatari zinazokukumba.
Kwa kuwa barakoa za hospitali ni chache, zinatakiwa kuhifadhiwa ili zitumiwe na:
wahudumu wa afya wanaowahudumia watu walio na dalili za COVID-19 watu wenye dalili za COVID-19 makundi yaliyo hatarini zaidi wakati ambapo kukaa mbali haiwezekani.
Barakoa za kimatibabu zinaweza kumlinda aliyevaa asipate COVID-19, lakini zinapaswa kutumika pamoja na mbinu nyingine za usalama, ikiwa ni pamoja na kunawa mikono mara kwa mara na kukaa mbali na wengine.
Barakoa za vitambaa zinapatikana zaidi, unaweza kuzitengeneza mwenyewe. Barakoa hizi zinafaa kwa watu ambao hawajaambukizwa kuzivaa katika maeneo ya umma. Zinazuia usisambaze virusi ikiwa una COVID-19 lakini hujatambua na huna dalili. Barakoa za vitambaa hazikuzuii (uliyevaa) usipate COVID-19, kwa hivyo hakikisha kuwa unazingatia mbinu nyingine – kujitenga na wengine na kunawa mikono yako ili kupunguza uwezekano wa kuapata COVID-19.
Ninawezaje kutumia barakoa kwa usalama?
Barakoa zinapaswa kutumika pamoja na mbinu nyingine za usalama, ikiwa ni pamoja na kukaa angalau umbali wa mita 1 kati yako na watu ambao huishi nao, kunawa mikono mara kwa mara na kupunguza mwingiliano wa kijamii.
Ili barakoa ikulinde ipasavyo inahitaji kukutosha vyema na isilegee. Inapaswa kufunika pua yako, mdomo na kidevu na unapaswa uweze kupumua kwa urahisi ukiwa umeivaa. Ufuatao ni ushauri kuhusu jinsi ya kutumia barakoa ipasavyo:
Kabla hujavaa barakoa, hakikisha kuwa mikono yako ni safi na barakoa si chafu na haijatoboka (kwa mfano ikiwa ina matundu).
Epuka kugusa barakoa unapokuwa umeivaa. Ukigundua kuwa barakoa imelowa au imechafuka, ibadilishe uvae nyingine.
Safisha mikono yako kabla ya kuvua barakoa yako. Tumia kamba za masikioni kuvua barakoa yako, zingatia usiguse sehemu ya mbele ya barakoa. Nawa mikono yako tena baada ya kuvua barakoa.
Usichangie barakoa yako na watu wengine. Wakati ambao huivai, iweke kwenye mfuko unaweza kufungwa upya. Ikiwezekana unapaswa kuosha barakoa yako katika maji ya moto na sabuni kila siku jioni.
Kibuyu chirizi ni nini na ninawezaje kulitengeneza?
Kibuyu chirizi ni kifaa rahisi kinachoweza kukusaidia uohse mikono yako na maji. Unaendesha kibuyu chirizi kwa mguu, ili usiguse vishikio vyovyote ambapo vijidudu, bakteria au virusi vinaweza kuishi. Unakanyaga wenzo na maji yanamiminika viganjani mwako.
Vibuyu hivi chirizi ni rahisi kutengeneza na ni njia bora ya kunawa miko yako ikiwa huwezi kupata maji tiririka au mabomba. Kuna njia mbalimbali za kutengeneza vibuyu chirizi Vitu vya msingi utakavyohitaji ni:
Chombo cha maji cha plastiki (chenye kishikio na kifuniko), kamba fimbo ndefu (moja kwa ajili ya wenzo na nyingine ikiwa unatengeneza fremu) Tawi au fremu iliyotengenezwa kwa fimbo ili kushikilia kibuyu chirizi kwa juu.
Kwa maagizo kamili kuhusu kutengeneza kibuyu chirizi, angalia mwongozo<a href="https://www.youtube.com/watch?v=URfDHHOv-YA"> huu. </a>