Je, unaweza kupata VVU kupitia manii inayotoka kabla ya shahawa?
Manii inayotoka kabla ya shahawa ina kiwango kidogo cha kuwa na VVU. Manii inayotoka kabla ya shahawa ni ute unaoonekana unaotoka kwenye uume kabla ya mwanamume kutoa manii. Kuna kiwango kidogo cha VVU katika manii inayotoka kabla ya shahawa kuliko ilivyo kwenye shahawa, lakini bado ipo. Hii ina maana kwamba njia ya kumwaga manii nje au ‘kutoa nje’ si njia ya kuaminika ya kuepuka kuambukizwa VVU.
Je, hatari ya kupata VVU kupitia ngono ni sawa kila wakati?
Hatari ya kupata VVU kutokana na ngono inaweza kutofautiana, kulingana na sababu kadhaa. Baadhi ya sababu hizi zinahusiana na aina ya ngono unayofanya, kwa mfano Ngono kupitia njia ya haja kubwa au ukeni zote zina hatari kubwa ya kuambukizwa VVU kuliko Ngono kwa njia ya mdomo. Sababu nyingine zinazohusiana na afya ya mhusika, kwa mfano ukiwa na magonjwa ya zinaa, uwezekano wako wa kupata VVU huongezeka. Mojawapo ya sababu ya hii ni kuwa magonjwa mengi ya zinaa husababisha michubuko ya ngozi ya sehemu za siri ambayo hupelekea VVU kupenya kwa urahisi. Vile vile, ikiwa mtu amepata VVU hivi karibuni, ana uwezekano mkubwa wa kuambukiza. Hii ni kwa kuwa Kiwango chake cha VVU kwenye damu kitakuwa juu katika awamu hizi za mwanzo za maambukizi. Kwa upande mwingine, ikiwa unafuata vizuri matibabu, hatari ya kuambukiza VVU huwa ni ndogo sana na hatimaye hupotea visipoonekana.
Ingawa ni vyema kujua ni mambo gani yanaweza kuongeza hatari ya mtu kuambukizwa au kupata VVU, njia hakika ya kudhibiti hatari yako ya kupata VVU ni kutumia kinga kama vile kondomu na Vidonge vya kumeza mara kwa mara vya kuzuia VVU (prEP).
Je, kuna chanjo ya VVU?
Hakuna chanjo ya kukuzuia kupata VVU. Ili kuepuka kupata VVU, unatakiwa kutumia njia ya kujikinga na VVU kama kondomu au PrEP na kuepuka kushiriki vifaa vyenye ncha kali. PrEP ni kidonge ambacho kinaweza kuzuia watu kupata VVU hata wanapofanya ngono bila kondomu na mtu mwenye VVU. PrEP ni nzuri sana katika kuzuia VVU lakini sio chanjo, kwa sababu ni lazima uendelee kutumia PrEP ili kujikinga. Mara tu unapoacha kutumia PrEP, hutaweza kujikunga tena dhidi ya VVU .
PrEP ya muda mrefu ya sindano ambayo itakulinda kwa muda mrefu (bila wewe kukumbuka kila siku) iliidhinishwa matumizi Marekani mapema mwaka wa 2022. Watafiti wanajaribu kutafuta njia ya kutoa chanjo dhidi ya VVU.