Boost

Lengo kuu la matibabu ni kuendelea kushusha kiwango cha VVU kwenye damu na hatimaye kupunguza kabisa makali ya virusi. Kiwango cha kuzingatia matibabu kinachohitajika ili kufikia hatua hii kinaweza kutofautiana kidogo baina ya watu, inaweza pia kutegemea dawa unazotumia na sababu nyingine za kibinafsi, kama vile iwapo una hali nyingine za kiafya.                                                                                                       Wahudumu wa kliniki kwa kawaida hutumia asilimia 95 ya uzingatiaji kama kiwango kinachohitajika cha kupunguza makali ya virusi. Hii humaanisha kuwa uzingatiaji wako unapaswa kukaribia asilimia 100, lakini usipozingatia dozi kwa muda fulani haitasababisha makali ya VVU yasipungue. Ukiendelea kusahau matibabu yako ya kupunguza makali ya virusi, utahitaji kuzungumza na mhudumu wa afya kuhusu hali hiyo. Ataweza kukusaidia.                                                                                                                        

Hushauriwi uache kupata matibabu yako kwa muda. Matibabu ya kupunguza makali ya VVU ni njia pekee ya kudhibiti VVU na kuimarisha mfumo wako wa kingamwili. Ni muhimu kuwa watu wanaoacha kupata matibabu ya kupunguza makali ya VVU waanze tena haraka iwezekanavyo. Iwapo uliacha kwa muda mrefu, unapaswa kumwona mhudumu wa afya kabla hujaanza tena. Atahitaji kukupima afya yako kwa ujumla na anaweza kupendekeza upate matibabu tofauti wakati huu.

Iwapo ni muhimu au si muhimu kutumia dawa za kupunguza makali ya VVU baada ya kula hutegemea aina ya dawa unazotumia. Sababu kuu ya mhudumu wa afya kukushauri kuhusu kula ni kwa kuwa chakula kinaweza kubadilisha namna dawa zako zinavyofyonzwa mwilini.                                           Kwa mfano, kutumia efavirenz baada ya kula chakula chenye mafuta mengi inaweza kusababisha kiwango cha dawa za kupunguza makali ya VVU kinachofyonzwa mwilini mwako kiwe kikubwa zaidi. Hii inaweza kufanya madhara ya dawa yawe mabaya zaidi na katika hali mbaya zaidi kusababisha kiwango cha dawa mwilini mwako ambacho kinaweza kuleta madhara. Dawa nyingine zinaweza kuhitaji ule chakula ii dawa zifyonzwe kikamilifu, kwa hivyo hakikisha unaelewa na kufuata maagizo ya mhudumu wako wa afya.                                                                                                                                                               Iwapo unatatizika kufuata ushauri kuhusu iwapo utumie dawa baada au kabla ya kula, mfahamishe mhudumu wako wa afya.