Boost

Kuna njia mbili kuu ambazo unaweza kutumia kupima VVU. Njia ya kwanza ni kupima damu yako ili kubaini antijeni za VVU. Antijeni ni sehemu ya nje inayozunguka virusi. Ni sehemu ya virusi vyenyewe. Kiwango kikubwa cha antijeni kinapobainika kwenye damu yako humaanisha kuwa una VVU.

Njia ya pili ni kupima kingamwili dhidi ya VVU. Kingamwili ni sehemu ya jinsi mwili wako unavyojikinga dhidi ya maambukizi. Ni seli ambazo mwili huzalisha ili kujingika na kujaribu kudhibiti maambukizi. Kuwa na kingamwili nyingi dhidi ya VVU kwenye damu ni dalili kuwa mwili wako umetambua maambukizi ya VVU na unajaribu kujikinga.

Vipimo vingi vitatumia muunganiko wa mbinu zote hizi, kupima kingamwili na antijeni. Upimaji unaojumuisha mbinu hizi ndio unaofaa kupima VVU kwa siku hizi.

'Vipindi vya kugundulika kwa VVU' hueleza muda unaochukua kati ya kupata VVU na kubainika kwenye vipimo.Kutakuwa na kuchelewa kati ya muda ambapo VVU huingia mwilini mwako na muda vinapobainika mwilini (au katika majimaji ya kinywani). Kwa maneno mengine, vipimo vya VVU haviwezi kuthibitisha kwa usahihi uwepo wa VVU hadi kipindi cha kugundulika kwa VVU kitakapokwisha. Muda wa kudumu kwa kipindi cha  kugundulika kwa VVU hutegemea aina ya kipimo kilichotumika.

Vipimo vya kingamwili vinaweza tu kutambua VVU miezi mitatu baada ya kuambukizwa. Hii ni kwa sababu mwili wako unahitaji muda kwanza ili kugundua VVU, kisha kuanza kutoa kingamwili. Kiwango cha kingamwili kinapaswa kuwa kikubwa sana ili kuwa na uhakika kwamba kitaonekana kwenye vipimo. Baada ya miezi mitatu asilimia 99 ya watu watakuwa na viwango vya kingamwili vya juu kuweza kugunduliwa katika vipimo.

Vipimo vya antijeni vina kipindi kifupi cha kugundulika kwa VVU. Vinaweza kugundulika kuanzia wiki nne baada ya kuambukizwa. Kipindi hiki cha kugundulika kwa VVU huruhusu VVU kuzaana vya kutosha kuweza kutambulika kwenye damu.

Iwapo unatumia Vidonge vya kumeza mara kwa mara vya kuzuia VVU (prEP) au Dawa zinazotumika baada ya kuwa katika hatari ya VVU (PEP) kipindi cha kugundulika kwa VVU kinaweza kuwa kirefu zaidi, kwa sababu dawa hizi zinaweza kuchelewesha utengenezaji wa kingamwili.