Boost

Ndiyo, manii inayotoka kabla ya shahawa inaweza kuwa na shahawa, ambayo inatosha kumfanya mtu awe mjamzito. Hii inamaanisha kuwa njia ya kumwaga nje si njia salama ya kuzuia ujauzito.

Kwa sababu manii inayotoka kabla ya shahawa haitoki kwenye korodani kuna uwezekano mdogo wa kuwa na manii ndani yake. Hata hivyo, inawezekana kwa manii inayotoka kabla ya shahawa kuchukua shahawa ambayo tayari iko kwenye mshipa wa urethra wakati wa kumwaga. Inathibitika pia kwamba baadhi ya wanaume huvuja kiasi kidogo cha shahawa kwenye manii inayotoka kabla ya shahawa. Kwa vyovyote vile, huwezi kuwa na uhakika ikiwa hakutakuwa na shahawa yoyote mtu anapotoa manii kabla ya shahawa, kwa hivyo ili kuepuka ujauzito ni muhimu kutumia njia nyingine ya kuzuia mimba.

Utoaji mimba hukomesha ujauzito baada ya mtu kupata mimba. Kuna njia tofauti za kutoa mimba. Kwa kawaida zinahusisha kutumia dawa au kufanya upasuaji mdogo. Ukigundua kuwa wewe ni mjamzito, lakini hutaki kujifungua mtoto, unaweza kufikiria kutoa mimba.

Fahamu kwamba katika baadhi ya nchi kunaweza kuwa na sheria zinazozuia utoaji mimba. Ni muhimu kuhakikisha kuwa utoaji wako wa mimba ni salama. Ni lazima ufanywe na mtaalamu wa matibabu aliyefundishwa katika hospitali maalum iliyo na leseni. Aina nyingine za utoaji mimba zinaweza kuwa hatari sana kwa wanawake.      

Hedhi ni sehemu ya mzunguko wa uzazi wa mwanamke, pia hujulikana kama mzunguko wa hedhi. Huu ndio mchakato ambao mwili wa mwanamke hupitia ili kujiandaa kwa ajili ya ujauzito. Ili kuwa tayari kwa ujauzito mambo kadhaa yanapaswa kutokea katika mwili wa mwanamke. Hizi ni hatua mbalimbali lakini kumbuka kuwa muda halisi utatofautiana kutoka kwa mwanamke mmoja na mwingine.

Siku ya 1 -5: Mzunguko huanza siku ya kwanza ya hedhi ya mwanamke wakati ambapo anaanza kutokwa na damu. Damu inayotoka ukeni imeundwa na uteute wa mji wa mimba. Ikiwa mwanamke si mjamzito, uteute mzito wa mji wa mimba ambao umejengwa kwa mwezi hauhitajiki na huanza kumeguka. Kisha uteute wa kwenye mji wa mimba lazima uondolewe, kwa namna ya kutokwa na damu. Kwa kawaida hedhi hudumu kati ya siku 2 na 7 kulingana na mtu.

Siku ya 5- 14: Karibu siku ya 5 ni wakati ambao kwa kawaida hedhi hukoma. Baada ya hedhi kumalizika mji wa mimba huanza kujiandaa tena kwa ajili ya mayai ya kutungisha mimba. Karibu siku ya 14, yai linalofuata linatolewa. Wanawake hutoa yai jipya kutoka kwenye ovari kila mwezi. Ni karibu katika siku ya 14 ambapo mwanamke ana uwezekano mkubwa wa kupata ujauzito.

Siku ya 15 -24: Yai ambalo limetolewa kwenye ovari husafiri kwenda chini ya mrija wa falopia ili kufika kwenye mji wa mimba, hali hii inaweza kuchukua siku kadhaa. Wakati huo huo, mji wa mimba unajiandaa kupokea yai. Wakati yai linapofika, uteute wa mji wa mimba wa mwanamke unapaswa kuwa mzito, ili kuwe na tabaka laini la tishu ambalo yai linaweza kupandikizwa ndani yake.

Siku ya 25-28: Ikiwa yai limerutubishwa na manii, linapofika kwenye mji wa mimba litapandikizwa kwenye uteute mzito wa mji wa mimba. Likiwa limewekwa kwenye uteute wa mji wa mimba, yai lililorutbishwa litahifadhiwa salama na litapata kila kitu kinachohitajika ili kukua. Katika hali hii, mzunguko wa kawaida wa hedhi unavurugwa na badala yake mimba huanza. Vinginevyo, ikiwa yai halijarutubishwa, litaanza kumeguka pamoja na uteute wa mji wa mimba. Mzunguko unaanza tena wakati kipindi kingine cha hedhi kinaanza.

Katika mzunguko wote wa hedhi wa kila mwezi, wanawake wanaweza kupata mabadiliko katika hisia zao na viwango vya nguvu au maumivu ya tumbo la chini, ulaini katika matiti yao au dalili zingine. Mabadiliko haya yanasababishwa na viwango vinavyobadilika vya homoni katika miili yao ambazo zinadhibiti mzunguko wa hedhi. Kwa wanawake, kujua jinsi mwili wako na hisia zako zinavyobadilika mwezi mzima kunaweza kukusaidia kuelewa mahali ulipo katika mzunguko wako.