Boost

Kutumia PrEP bila kujua hali yako ya VVU ni hatari kwa afya yako. PrEP zina kiwango kidogo cha dozi ya Dawa za Kupunguza Makali ya VVU . Ukizingatia vizuri, kiwango hiki cha dawa za Kupunguza Makali ya VVU kinatosha kuzuia usipate VVU, lakini iwapo tayari una VVU inaweza kufanya mwili wako usikubali dawa ya VVU. Hii ni pale dawa zako za Kupunguza Makali ya VVU huacha kufanya kazi. Kiwango kidogo cha dawa hizo hakitoshi kuzuia virusi visiongezeke, badala yake, VVU vinaweza kujibadilisha ili kuepuka makali ya dawa na kuendelea kujizalisha.                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                       Kupima mara kwa mara  wakati unatumia  PrEP humaanisha kuwa utafahamu hali yako ya VVU haraka iwezekanavyo, ili uepuke mwili wako kukataa dawa ya VVU. Kutumia PrEP kama ulivyoelekezwa itazuia usipate VVU. 

Ndiyo! PrEP hazikuzuii usipate mimba na ni salama kwa wanawake kutumia wakati wa kubeba mimba, ujauzito na wanaponyonyesha. PrEP ni moja ya njia ambazo wapenzi walio na hali tofauti za VVU wanaweza kujaribu kupata mtoto kwa njia salama.                                 

Iwapo unataka kupata mtoto, lakini unafikiri kuwa upo katika hatari kubwa ya kupata VVU, basi PrEP zinaweza kuwa chaguo linalokufaa. Iwapo kina mama watapata VVU wakati wa ujauzito na kunyonyesha, huwaweka hatarini zaidi watoto wao. Hii ni kwa sababu Kiwango chao cha VVU kwenye damu kinakuwa kikubwa katika wiki kadhaa za mwanzo baada ya kupata VVU. Kutumia Dawa kabla ya kuwa katika hatari ya VVU hukulinda wewe na mtoto wako, ili msiwe na VVU katika kipindi chote cha kupata mimba, ujauzito na kunyonyesha.  

Watu huwa na hali tofauti wanapotumia PrEP. Watu wengi hawapati madhara, ingawa watu wengine wanaweza kuwa na hali ya kichefuchefu, kutapika, uchovu na kizunguzungu, lakini mara nyingi hali hizi hupotea baada ya wiki moja au mbili. 

Madhara ya muda mrefu ya kutumia PrEP ni machache. Takribani asilimia 2 ya watumiaji huenda wakapata matatizo ya figo, lakini hali ya kawaida hurejea ukimaliza kutumia PrEP. Ndiyo maana inashauriwa watu wanaotumia PrEP wapime afya mara kwa mara ili wahudumu wa afya wafuatilie afya zao.  

Iwapo mtu anahisi madhara yanayotokana na PrEP, anapaswa kuzungumza na mhudumu wa afya.