Boost

Iwapo majibu ya vipimo vyako vya mlango wa kizazi vitaonyesha kuwa si vya kawaida, utashauriwa kuhudhuria miadi mingine, inayoitwa coloposcopy. Hii itawapa wahudumu wa afya nafasi ya kuchnguza mlango wako wa kizazi. Wanaweza kuona zilizo seli zisizo za kawaida na matibabu yatakayokufaa. Kwa kawaida watachukua sampuli kwenye mlango wako wa kizazi ili wapime zaidi.  

Kulingana na hali yako, matibabu utakayopewa yatakuwa tofauti. Mara nyingi yanahusisha kuondoa au kuharibu seli zisizo za kawada. Seli zisizo za kawaida zikiondolewa, hazitaweza kubadilika na kuwa saratani - kwa hivyo unaweza kuendelea kuishi kama kawaida.                                                                                      

Mara nyingi seli zisizo za kawaida zinaweza kuondolewa bila upasuaji. Madaktari wanaweza kutumia waya mwembamba unaotumia umeme mdogo ili kuondoa seli zisizo za kawaida.    Kwa kutumia speculum waya huingizwa kupitia uke. Mchakato huu ni salama zaidi na kwa kawaida huchukua dakika 15. Utapewa dawa ya ganzi ili kukusaidia usihisi maumivu. Unaweza kurejea nyumbani baada ya matibabu haya, lakini kuwa na sodo ya kujizuia, kwa kuwa kunaweza kuwa na damu inayotoka mwanzoni baada ya matibabu. Ili kuepuka maambukizi, inashauriwa kuwa usitumie kisodo cha kunyonya majimaji ukeni ambacho huingizwa ukeni au kufanya ngono kwa wiki 4 baada ya utaratibu huo.     

Njia nyingine ni kuharibu seli kwa kuzichoma au kuzigandisha. Hii inaweza kufanyika kwa kutumia leza au kifaa cha kupimia cha baridi au chenye joto. Matibabu  haya yanaogofya lakini ni ya uhakika na hupaswi kuhofia. Huenda utahisi maumivu, kama ambavyo unaweza kuhisi unapokuwa kwenye hedhi. Baada ya utaratibu kukamilika utaweza kurejea nyumbani.

Lengo la kupima mlango wa kizazi ni kutambua seli zisizo za kawaida kabla hujapata saratani ya mlango wa kizazi. Hii humanisha kuwa unaenda kupima unapokuwa na afya njema na husubiri dalili zionekane.                                                                                                                                                                                                                                                                     Hata hivyo, ukigundua dalili zozote kati ya zifuatazo, ni lazima uzungumze mtoa huduma za afya:                                               a) kutoka damu ukeni isivyo kawaida                                           b)maumvivu au kuhisi vibaya wakati wa kufanya ngono   c)mabadiliko katika majimaji ya ukeni                                         d)maumivu katika eneo la katikati ya mifupa ya mapaja(kiwambo).                                                                         Ingawa hizi zinaweza kuwa dalili za mapema zaidi za saratani ya mlango wa kizazi, pia ni dalili za kawaida za matatizo mengine ya kiafya, kwa hivyo ni vyema uzungumze na mhudumu wa afya ukigundua mabadiliko haya.