Boost

Matibabu ya kudhibiti VVU baada ya kuzaliwa ( au tiba ya kudhibiti VVU baada ya kujifungua) ni aina ya Dawa zinazotumika baada ya kuwa katika hatari ya VVU (PEP) inayoweza kupewa kwa watoto wacha ili kupunguza uwezekano wao wa kupata VVU. Tiba hiyo inatolewa kwa watoto wachanga walio katika hatari ya juu ya kuambukizwa. Hii inahusisha pale ambapo kina mama wamepata VVU wakati wa ujauzito au kunyonyesha, wamechelewa kugundulika au wametatizika kuzingatia matibabu na wana kiwango cha juu cha virusi kwenye damu.                                                                                                                                                                     Watoto wengi watapewa dozi ya kila siku ya mchanganyiko wa zidovudine (AZT) na  navirapine (NVP) kwa wiki sita baada ya kuzaliwa. Kwa watoto wachanga wanaonyonyeshwa wataendelea kutumia dozi za AZT na NVP au NVP pekee kwa wiki 6 zaidi.     Baada ya wakati huo kiwango cha virusi cha mama kinapaswa kuwa kimepungua ili mtoto aendelee kunyonya, bila kuhitaji kinga yoyote ya ziada.            

Ni muhimu kuwa, baada ya mtoto mchanga kuacha kutumia tiba ya kudhibiti VVU baada ya kuzaliwa asianze tena, hata kama kiwango cha virusi kwenye damu ya mama kitaongezeka. Badala yake anapaswa kupata ushauri kutoka kwa wahudumu wa afya kuhusu kuzingatia matibabu na kukabiliana na vikwazo vyovyote vya kuzingatia matibabu.

Ubongo wa mtoto hukua kwa haraka zaidi katika siku 1,000 za kwanza baada ya kuzaliwa (takribani miaka 3 ya kwanza). Watoto wachanga hukua vyema wakiwa na vitu vyote vilivyoorodheshwa hapo chini.

1. Huduma ya afya - afya duni inaweza kuathiri hatua za mwanzo za ukuaji wa mtoto. Kuhakikisha kuwa anapata mahitaji yake ili afya yake iimarike, ikiwa ni pamoja na chanjo na matibabu ya ugonjwa wowote itafanya afya duni isiathiri ukuaji wake. 
2. Lishe - mtoto wako mchanga anahitaji mlo sahihi ili akue. Maziwa ya mama yanaweza kuwapatia watoto wachanga virutubisho vyote wanavyohitaji ili kukua katika miezi yao 6 ya kwanza. Unaweza kuamua kumnyonyesha muda mrefu zaidi ya huo.                                                
3. Usalama - mazingira salama na malezi, ambapo watoto wachanga wanapewa upendo wa kutosha na familia zao husaidia ukuaji wao. Kuwa katika mazingira ya vurugu, kutokuwa na uangalizi au migogoro  inaweza kupunguza uwezo wa mtoto kukua akiwa na afya.               

4. Utunzaji sahihi - michezo na kushiriki na wengine husaidia ukuaji wa mtoto. Ni muhimu kwa watoto wachanga wapate utunzaji sahihi wanaohitaji kutoka kwa watu wazima. Kutabasamu, kuwatazama, kuzungumza na kuwaimbia, yote humsaidia mtoto wako ajifunze na akue.                                                                                                                                           5. Mafunzo ya mapema - watoto wanapokua ni muhimu kuwa fursa hizi za kujifunza ziendelee. Wanapaswa kupelekwa chekechea au sehemu zingine ambazo wanaweza kujifunza.